Thursday, January 27, 2011

SARAH ARUDI NA USHINDI KUTOKA MALI


Mwanariadha wa  kike SARAH BONIFACE ambaye amshika nafasi ya kwanza  katika mbio za kilometa kumi  za mashindano ya riadha ya kimataifa ya benki ya AFRIKA BOA zilizofanyika huko BAMAKO nchini  MALI amesema kuwa  hali hewa iliwapa tabu lakini ameweza kuliwakilisha vyema TAIFA.

SARAH amesema kuwa mbio hizo zilikuwa na ushindani mkubwa huku mwenyekiti wa benki ya BOA FULGENCE KAZAURA akifurahia mafanikio ya mwanariadha huyo.

Mchezaji huyo alitumia muda wa dakika 35 ,sekunde 52 na nukta 20 ambapo mkimbiaji mingine wa kiume MASHAKA MASUMBUKO ambaye alikimbia  kilometa 42 alishindwa kumaliza mbio hizo kutokana na kupata tatizo la misuli.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU