Thursday, January 27, 2011

KOCHA WA TIMU YA DEDEBIT ASEMA AJA KUIMALIZA YANGA,MCHEZO KUFANYIKA JUMAMOSI UWANJA WA TAIFA

                                   Kocha wa timu ya DEDEBIT GEBREMEDHIN HAILE
Baadhi ya wachezaji wa DEDEBIT wakiwa hoteln

Kocha wa timu ya klabu ya DEDEBIT ya ETHIOPIA amesema kuwa amekuja kushindana na YANGA , na kuwa anaiilewa vyema timu hivyo wamejiandaa kuibuka na ushindi.

Akizungumza i jijini DSM, kocha huyo GEBREMEDHIN HAILE amesema   amekaa na timu hiyo kwa muda wa siku  kumi , lakini ameiandaa vizuri katika mchezo huo.

Kocha HAILE ambaye kabla ya kujiunga na kikosi hicho alikuwa akifundisha katika klabu iliyopo nchini YEMEN amesema kuwa YANGA ni timu kubwa yenye uzofu mkubwa kwani timu yake ndio mara kwanza kucheza mashindano kama hayo na inashika nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi nchini ETHIOPIA.

Hata hivyo ,kocha HAILE amesema timu yake haijapata mechi za majaribio za kimataifa ,ambapo imeweza kucheza michezo mbali mbali na timu za ETHIOPIA tu.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU