Monday, January 24, 2011

ASHA ATUA UTURUKI KWA ,KUSAINI MKATABA WA MWAKA MMOJA NA NUSU IWAPO ATAFUZU MAJARIBIO

                                       ASHA akipanda gari la timu yake


                                         ASHA akiwa chumbani kwake
                                    akiwa na wachezaji wenzake
akipata msosi
MChezaji wa kutumainiwa wa timu ya taifa ya wanawake ya TANZANIA ambaye pia huchezea klabu ya MBURAHATI QUEENS, ASHA RASHID maarufu MWALALA anafanyiwa  vipimo vya afya  nchini UTURUKI  katika hatua za mwisho za  kujiunga na timu ya ATASEHIR BELEYEDISPOR ambayo inshiriki katika ligi kuu ya soka ya wanawake nchini humo.

ASHA ambaye aliwasili nchini UTURUKI mwishoni mwa wiki iliyopita alitumiwa wito wa kufanyiwa majaribio na timu hiyo pamoja na mchezaji mwingine wa timu ya JKT QUEENS ,ETO MLENZI .

Wakala wa FIFA na golikipa wa zamani wa timu ya taifa ya UTURUKI AHMET ARIC ndiye aliyewaona wachezaji hao kupitia video za mtandao wa YOUTUBE na kuwaunganisha kwa meneja wa timu hiyo MURAT ULKU.
ASHA ambaye ameanza mazoezi mepesi na timu hiyo amesema ana matumaini ya kufanya vizuri na kusajiliwa na timu hiyo , ambapo mashabiki wa timu hiyo wameonekana kumfurahia .

Kwa mujibu wa Mwandishi wa kujitegemea wa habari  za michezo ,NISHA LIGON ni kwamba taratibu za safari ya ETO bado zinasubiri ruhusa kutoka kwa mwajiri wake ambaye ni JESHI LA KUJENGA TAIFA –JKT.



0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU