Sunday, January 23, 2011

SIMBA YAKUBALI YAISHE KWA AZAM YACHAPWA MAGOLI MATATU KWA MAWILI


Mabingwa watetezi SIMBA , wameanza mzunguko wa pili wa ligi kuu soka TANZANIA BARA kwa kucharazwa na AZAM FC kwa magoli MATATU kwa MAWILI katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa TAIFA  jijini DSM.

Katika mchezo huo , SIMBA walikuwa wakwanza kupata goli kupitia kwa mchezaji wake NICODEMUS NYAGAWA , goli ambalo lilisawazishwa na JOHN BOKO.

Goli la pili la AZAM FC lilipachikwa tena na JOHN BOKO kabla ya goli la tatu la timu hiyo kupachikwa na mshambuliaji MRISHO NGASSA.

Goli la pili la simba lilipachikwa na HILARY ICHESA wakati zikiwa zimesalia dakika tatu mpira kumalizika, hivyo basi hadi mwisho wa mchezo SIMBA MBILI wakati AZAM FC ikitoka kifua mbele kwa magoli yao MATATU na pointi TATU.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU