Monday, May 9, 2011

HATIMAYE BFT YASALITI AMRI YA KUWAREJESHA MABONDIA WAZOEFU

Hatimaye shirikisho la ngumi za ridhaa nchini BFT limekubali ombi la kocha wa timu ya ngumi la kuwarejesha wachezaji waliochwa katika kikosi cha timu hiyo kinachoajiandaa na mashindano ya AFRIKA MASHARIKI na KATI yatakayofanyika nchini UGANDA mwezi ujao.
Makamu mwenyekiti wa BFT MICHAEL CHANGARAWE amesema kuwa uamuzi huo umefikiwa kutokana na kikao cha kamati ya utendaji kilichokaa hivi karibuni ambapo ameeleza kuwa wameshawataarifu wachezaji hao .

CHANGARAWE amesema kuwa kutokana na kuhitaji kupata medali katika mashindano hayo ya kimataifa , uamuzi huo utaweza kusaidia katika kuwa na wachezaji wenye uzoefu wakichanganyika na wachezaji chipukizi
Baadhi ya wachezaji hao ni pamoja na nahodha wa timu ya taifa JOSPEH MARTIN, NASSER MAFURU, ambao waliachwa kwenye timu ya taifa kutokana na kugomea kucheza michuano ya kimataifa iliyofanyika nchini mwaka jana na pia kutofanya vyema katika michuano ya jumuia ya madola.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU