Kushoto ni kocha wa timu ya AFRIKA KUSINI BAFANA BAFANA PITSO MOSIMANE katikati mwakilishi wa shirikisho la soka AFRIKA KUSINI na kulia ni kocha wa STARS JAN PAULSEN wakizungumza Jijini DSM katika ukumbi wa TFF.
MAKOCHA wa timu za Taifa za AFRIKA KUSINI, BAFANA BAFANA na TANZANIA TAIFA STARS leo wamekutana na waandishi wa habari kuzungumzia mchezo wao wa kirafiki wa kimataifa huku kocha wa BAFANA BAFANA akiweka wazi kuwa anaiheshimu sana TAIFA STARS na katu hatoidharau katika pambano hilo.
Kocha PITSO MOSIMANE anasema amekuja na kikosi kitakachoongozwa na nahodha msaidizi MORGAN GOULD badala ya SIPHIWE SHABALALA ambaye hajaambatana na kikosi hicho kwa kuwa timu yake ya KAIZER CHIEF inakabiliwa na mechi muhimu katika ligi kuu ya AFRIKA KUSINI.
Kocha PITSO MOSIMANE anasema amekuja na kikosi kitakachoongozwa na nahodha msaidizi MORGAN GOULD badala ya SIPHIWE SHABALALA ambaye hajaambatana na kikosi hicho kwa kuwa timu yake ya KAIZER CHIEF inakabiliwa na mechi muhimu katika ligi kuu ya AFRIKA KUSINI.
BAFANA BAFANA itawakosa wachezaji wake NANE muhimu wakiwemo kina SIPHIWE SHABALALA,ITUMELENG KHUNE na STEVEN PIENAR huku kocha MOSIMANE akiwataja wachezaji kama MRISHO NGASSA , JUMA KASEJA,STEPHANO MWASIKA na SHADRACK NSAJINGWA kuwa ni wachezaji anaowahofia kwa TAIFA STARS .
kwa upande wake kocha wa TAIFA STARS , JAN PAULSEN anasema TAIFA STARS inakabiliwa na wachezaji wawili majeruhi ambao hawatakuwepo katika mchezo huo wa kesho ambao ni mlinzi wa kushoto STEFANO MWASIKA na winga MRISHO NGASSA.
Timu ya AFRIKA KUSINI ipo nafasi ya 39 kwa ubora wa soka duniani huku TANZANIA ikiwa nafasi ya 112.
Timu mbili hizi zinakabaliwa na michezo wa kimataifa wa kutafuta tiketi ya kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Afrika zitakazofanyika EQUATORIA GUINEA na GABON mapema mwakani.
TAIFA STARS na BAFANA BAFANA zote zitacheza ugenini ambapo TAIFA STARS itacheza na JAMHURI ya AFRIKA ya KATI, wakati BAFANA BAFANA itacheza na mapharao wa MISRI.
0 maoni:
Post a Comment