Friday, May 13, 2011

MWENYEKITI YANGA AMUONYA MWENYEKITI WA SIMBA ISMAIL ADEN RAGE KUWA ASIWE MSEMAJI WA YANGA

Kushoto msemaji wa YANGA LOUIS SENDEU na mwenyekiti wa YANGA NCHUNGA akiongea na waandishi klabuni YANGA juu ya kucheza mchezo wa kimataifa na timu ya BIRMINGHAM CITY kwa kudai kuwa hawajafikiana na klabu ya SIMBA
               Viongozi wa BIRMINGHAM walipotembelea uwanja wa Taifa na kukagua vyumbani
KLABU ya YANGA imetilia mashaka ujio wa klabu ya BIRMINGHAM CITY ya ENGLAND baada ya kuwepo kwa SINTOFAHAMU kati ya mawasiliano ya Mwenyekiti wa klabu ya SIMBA-ISMAIL ADEN RAGE na wakala wa mchezo huo pamoja na fedha inayotakiwa kukusanywa ndani ya miezi miwili ili kuilipa timu hiyo iweze kuja hapa nchini.

Kwanza Mwenyekiti wa klabu ya YANGA, LLOYD NCHUNGA ameshangazwa na Mwenyekiti wa SIMBA, ISMAIL ADEN RAGE kuwa msemaji wa klabu ya YANGA katika suala la ujio wa timu ya BIRMIGHAM CITY na kudai kuwa YANGA hawakukubali kucheza mchezo huo kutokana na vikwazo vilivyojitokeza.

NCHUNGA, ameshangazwa na kikwazo cha awali kwamba kama timu hiyo itakuja nchini lazima ipatiwe kiasi cha zaidi ya shilingi BILIONI MBILI.

Mahitaji mengine ni suala la kupewa fedha kiasi cha dola laki TATU ikiwa ni ada ya wakala wa mchezo huo , na kuwepo na fedha ya ziada isiyokuwa na maelezo ambayo ni dola LAKI MOJA.

Pamoja na masuala hayo pia kuna mahitaji mengine makubwa ambayo ni ULINZI , usafiri wa ndege wa daraja la BUSSINESS kwa timu ya BIRMIGHAM CITY,wanatakiwa walipiwe malazi katika hoteli ya nyota tano,kupatiwa bima ya afya pamoja na usafiri wa ndani.

Timu hii ya BIRMINGHAM CITY inataraji kucheza mechi mbili dhidi ya SIMBA na YANGA na tayari wakaguzi wao wakiongozwa na kocha wao msaidizi  ANDREW WATSON na Daktari wa timu hiyo IAN Mc GUINESS wameshakuja nchini kukagua uwanja wa TAIFA na hoteli watakayofikia.

Gharama zote hizi ni zaidi ya shilingi BILLIONI MBILI ambao ni mzigo unaotakiwa kulipwa na timu za SIMBA na YANGA huku vilabu hivi vikitegemea viingilio vya mapato ya uwanjani ili kurudisha gharama hizi.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU