Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen ataingoza timu hiyo kwenye mechi yakirafiki dhidi ya Afrika Kusini (Bafana Bafana) itakayochezwa Mei 14 mwaka huuUwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 12 kamili jioni.Awali Poulsen ambaye pia ni mkufunzi wa makocha alikuwa ameteuliwa na Shirikishola Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kuendesha kozi ya makocha nchini Gambia Mei 6- 14 mwaka huu. Kozi hiyo imeahirishwa hadi Septemba mwaka huu.
Kikosi cha wachezaji 19 wa Stars kinaingia kambini kesho (Mei 7 mwaka huu)hoteli ya Atriums jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi hiyo ambayoinazikutanisha timu hiz kwa mara ya kwanza.
Wachezaji walioitwa na Poulsen kwa ajili ya mechi hiyo ni makipa Shabani Kado(Mtibwa Sugar), Shaaban Dihile (JKT Ruvu) na Juma Kaseja (Simba). MabekiniShadrack Nsajigwa (Yanga), Aggrey Morris (Azam), Nadir Haroub ‘Cannavaro’(Yanga), Amir Maftah (Simba),
Juma Nyoso (Simba) na Kigi Makasi (Yanga).Viungo ni Nurdin Bakari (Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Jabir Aziz(Azam), Ramadhan Chombo ‘Redondo’ (Azam) na Mwinyi Kazimoto (JKT Ruvu).Washambuliaji ni Machaku Salum (Mtibwa Sugar), Mrisho Ngasa (Azam), MohamedBanka (Simba), John Bocco (Azam) na Mbwana Samata (Simba).
Wachezaji wanaocheza nje ambao wataanza kuripoti wiki ijayo ni Idrissa Rajab(Sofapaka, Kenya), Henry Joseph (Kongsvinger IL, Norway), Abdi Kassim (DT LongAn, Vietnam), Dan Mrwanda (DT Long An, Vietnam), Nizar Khalfan (VancouverWhitecaps, Canada) na Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden).
0 maoni:
Post a Comment