Thursday, May 5, 2011

MIPIRA WA MIKONO MUUNGANO KUANZA MEI 15 MWAKA HUU

Michuano ya mpira wa mikono ya muungano imepangwa kufanyika mei 15 mwaka huu katika uwanja wa ndani wa TAIFA.

 
Katibu mkuu wa chama cha mchezo wa mipira wa mikono nchini NICOLAUS MIAYO amesema mashindano hayo ya mpira wa mikono yatashirikisha timu kutoka TANZANIA BARA na TANZANIA VISIWANI.

Amesema mbali na timu kutoka DSM lakini zingine zitatoka katika mikoa ya MBEYA na RUVUMA mjini SONGEA akiwemo MAGEREZA zote wanawake na wanaume.

MIAYO amezitaja timu shiriki katika mashindano hayo kwa upande wa bara ni JKT,MAGEREZA,NGOME,DAR STARS zote wanawake na wanaume.

Lakini pia katibu MIAYO amezitaka timu shiriki katika mashindano hayo kufanya maandalizi ya kutosha na si kuleta malalamiko mara baada kuona zimefanya vibaya katika michuano hiyo.

Bingwa mtetezi katika michuano hiyo ya muungano ni MAGEREZA .




0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU