Warembo wapatao therathini wanategemea kuchujwa hadi kufikia idadi ya washiriki kumi na mbili ambao watapanda jukwaani kuchuana katika kinyang"amyiro cha kumsaka mlimbwende wa mkoa wa kilimanjaro 2011.
Shindano hilo ambalo liko katika maadalizi mazuri kupitia kamati yake ambayo siku ya Jumamosi hii watachuja warembo hao ili kupata idadi kamili inayoitajika na kupata warembo bora ambao wataongeza msisimuko wa mashindano hayo kama ilivyodhumuniwa na kamati hiyo.
Msemaji wa mashindano hayo Bw. Methusela Magese amesema kuwa tarehe ya mashindano imebadilishwa na sasa shindano hilo litafanyika tarehe 18 juni katika Hotel ya Salsanero iliyoko shant town mjini moshi.
Mashindano ya kutafuta mrembo wa TANZANIA yameaza kwa kasi kubwa baada ya kufanyika kwa uzinduzi hapa jijini DSM
0 maoni:
Post a Comment