Monday, May 2, 2011

KAMPUNI YA VIFAA VYA MICHEZO YA GIVOVA KUTOKA ITALIA YAANZA MAZUNGUMZO NA TFF KUDHAMINI TIMU ZA TAIFA

              Mmoja wa wafanyakazi kutoka benki ya NMB pamoja na mwakilishi kutoka kampuni ya GIVOVA wakifungua vifaa vya michezo ambayo huenda vikaanza kutumika hapa nchini iwapo makubaliano yatafanyika na TFF
 Kocha wa timu ya TAIFA TAIFA STARS JAN PAULSEN kushoto akiwa na mwakilishi kutoka kampuni ya GIVOVA kutoka ITALIA CORNELUS EHIMIAGHE katikati pamoja na katibu wa TFF ANGETILE OSEAH wakati wa utambulisho wa kampuni hiyo Jinini DSM
                                            EHIMIAGHE akionyesha moja ya jezi inayotengeneza kampuni hiyo
                                                           vifaa vya michezo kutoka GIVOVA
                                          Hapa ni moja ya track suti kwa ajili ya wachezaji pamoja na watu wengine.


Kampuni ya kimataifa ya kutengeneza vifaa vya michezo ya GIVOVA inafanya mazungumzo na Shirikisho la soka hapa nchini (TFF) pamoja na wadau ili kutoa udhamini kwa timu za soka za taifa.

Mwakilishi wa kampuni hiyo kutoka nchini ITALIA CORNELIUS EHIMIAGHE amesema lengo ni kuinua soka la TANZANIA na endapo Kampuni hiyo itaingia makataba na TFF itatoa huduma nyingine zikiwa ni elimu ya usimamizi wa michezo, fedha, pamoja na vifaa kwa timu zote za taifa ikiwamo timu za vijana na ile ya wanawake.


Kampuni hiyo  imekuwa ikizifadhili timu mbalimbali zinazoshiriki ligi kuu ya ITALIA na BARANI ULAYA vikiwamo vilabu vya CATANIA na CHIEVO na pia kuifadhili timu ya taifa ya visiwa vya MALTA ambayo inawania fainali za kombe la mataifa barani ulaya hapo mwakani.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU