Monday, May 2, 2011

TIMU YA BIRMINGHAM KUTOKA UINGEREZA KUTUA NCHINI

Vilabu vya SIMBA na YANGA huenda vikapata nafasi ya kucheza mechi za kirafiki za kimataifa na timu ya BIRMINGHAM CITY ya nchini UINGEREZA iwapo viongozi wa timu hiyo watakapokuwa wameridhishwa  na uwanja wa TAIFA pamoja na HOTEL ya KEMPINSKI anbayo timu hiyo itafikia.

Iwapo viongozi huo utafurahishwa na kiwango kinachotakiwa kwa uwanja na hotel basi SIMBA na YANGA zitajitupa uwanjani ambapo mchezo kati ya  SIMBA na BIRMINGHAM utafanyika JULAI 7 wakati mchezo na YANGA utafanyika JULAI 12 katika uwanja wa TAIFA.

Ujio wa timu ya BIRMINGHAM kutoka UINGEREZA umethibitishwa na mwenyekiti wa SIMBA ISMAL ADEN RAGE kuwa mipango yote imekamilika wanasubiri ukaguzi wa  viongozi hao akiwemo Kocha msaidizi pamoja na daktari mkuu wa timu hiyo na mara baada ya kukamilika wanatarajia kuja na mashabiki zaidi ya elfu moja pamoja na waandishi wa habari

Timu ya BIRMINGHAM ipo nafasi ya kumi na tano na inapointi thelathini na tisa katika msimamo wa ligi ya ENGLAND

KUHUSU MAJENGO YA SIMBA

RAGE amesema wapangaji katika majengo ya SIMBA wamepewa siku mbili kusaini mkataba mpya na viongozi wa SIMBA na si vinginevyo la sivyo sheria inachukua hatua .

 WACHEZAJI MGOSI NA YONDANI.

KERVIN YONDANI ameandika barua ya kuomba radhi kwa kutooneka klabuni hapo lakini barua yake bado kamati ya utendaji haijakaa kujadili iwapo amesamehewa ama la,kwa upande wa mchezaji MUSSA HASSAN MGOSI RAGE amesema barua ya mchezaji huyo haijajitoshereza kwa majibu hivyo amepewa nafasi nyingine ya kujieleza tena kwanini asichukuliwe hatua za kinidhamu.

Wachezaji hao mpaka sasa wanapata mshahara nusu huku mchezaji MUSSA HASSAN MGONI barua yake ikitupwa nje na anatakiwa kujieleza upya kwani maelezo hayajajitosheleza.

Wachezaji hao wamekuwa wanalipwa nusu msharaha kutoka na utovu wa nidhamu walionyesha wakati wa ligi kuu TANZANIA BARA.

Katika hatua nyingine mkutano mkuu wa SIMBA umepangwa kufanyika MEI  mwaka huu kama katiba inavyosema.

0 maoni:

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU