Sunday, January 23, 2011

MINZIRO AANZA KAZI YANGA

                                             MINZIRO NA PAPIC baada ya mazoezi
                                    Baada ya mazoezi wachezaji wa YANGA wakiomba
KOCHA msaidizi wa timu ya YANGA, FRED FELIX MINZIRO ameanza kazi rasmi ijapokuwa ijapokuwa mwandishi wa TBC amemshuhudia kocha huyo akiwa amekaa nje ya uwanja hadi kocha KOSTADIN PAPIC alipomaliza mazoezi yake naye kujuika na wachezaji kwa sala ya kufunga mazoezi ya siku.

Wakati wanamaliza mazoezi hayo kocha MINZIRO amekiri kwamba ni faraja kwake kufundisha pamoja na kocha PAPIC na yeye mbali na kusaidia masuala ya kiufundi pia atasaidia suala la SAIKOLOJIA katika timu hiyo.

MINZIRO ni miongoni mwa wachezaji wa zamani waliowahi kuchezea timu ya YANGA na kufundisha timu hiyo katika nyakati tofauti.

1 maoni:

Shein Rangers Sports Club said...

Tunamtakia kila la heri katika kazi yake mpya.

Post a Comment

WANAOTEMBELEA KWA SIKU